ASILIMIA 75 ya Watanzania wanaoishi vijijini hutegemea kilimo.Asilimia 80 ya matumizi ya nishati vijijini Tanzania ni kuni na mkaa, pia Dar es Salaam peke yake ina takribani watu milioni 5 ambapo wastani 70% ya wakazi hutumia mkaa kupikia. Inasemekana kwamba kuzalisha tani 590,000 za mkaa kwa mwaka hutumia tani 3,000,000 za miti na kusababisha hasara ya ukataji miti kwa kiwango cha zaidi ya hekta 100000 kwa mwaka.
Kumekuwa na jitihada mbalimbali za kupambana na matumizi ya kuni zinazofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Mojawapo ya wadau hao ni Space Engineering Co Ltd, kampuni iliyoanzishwa 1991 Jijini Dar Es Salaam ikiwa na waanzilishi watatu ambao azma yao kubwa imekuwa ni kuzalishwa majiko na mkaa kulingana na mahitaji ya wahitaji.
Aidha kampuni hii pia imekuja na mpango wa kutoa majiko bura kwa mama ntilie kwa makubaliano kwamba wawe wananunua mkaa mbadala kutoka kwao. Tofauti na makampuni mengine, kampuni hii imejikita mizizi kuhakikisha pamoja na jamii nyingine, lakini wale wa hali ya chini wanawezeshwa kutumia teknolojia ya mkaa mbadala.
Mwaka 2018 kampuni hii ilishiriki mashindano ya Mkaa Mbadala yaliyoendeshwa na Shell Exploration and Production Tanzania kwa kushirikiana na ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) yaliyolenga kuhamasisha utunzaji mazingira nchini, ambapo waliibuka nafasi ya pili kwa kupata Sh100milioni pamoja na ushauri kutoka taasisi ya IMED; Institute of Management and Entrepreneurship Development.
Lengo la mradi ni kueneza teknolojia bora ya nishati ya kupikia kwa kutumia mabaki ya misitu na taka za kilimo kuzalisha mkaa taka (briquettes). Pia kukuza nishati mbadala na mazingira endelevu. Teknolojia hii ya kutengeneza mkaa taka na majiko sanifu itakapoboreshwa itaharakisha maendeleo nchini hasa katika matumizi ya nishati majumbani na kibiashara,
Kampuni hiyo inawalenga wateja wa hali ya chini na kati kiuchumi wakiwamo wafanyabiasha wa chips (wakaanga chips). Kutumia nishati hii maana yake ni kubana matumizi ya nishati nyingine hasa mkaa wa kuni ambao ndio umekuwa ukitumika zaidi kabla ya kuibuliwa kwa aina hii mpya ya mkaa, kwa hiyo una manufaa kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa wanaofanya biashara ya vyakula.
Space Engineering Co Ltd tayari imeshatengeneza majiko sanifu ambayo yamegawanywa kwenye kantini za vyuo mbali mbali Dar es Salaam ikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika hosteli za JPM, Chuo cha Maji, Chuo cha DUCE, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), ambako pia wamekuwa wakisambaza mkaa mwingi.
Anasisitiza kuwa, “Changamoto tunazokutana nazo sokoni ni nyingi ila tunajitahidi kupambana nazo kama gesi, kuni, Mkaa wa kuni n.k, hawa tunapambana nao kwa kuongeza ubora wa bidhaa yetu,kuwajali wateja ikiwa ni pamoja na kuwatembelea mara kwa mara kujua kama kuna matatizo, na kufanya huduma kwenye majiko yao. Pia tunajitahidi kuhakikisha wateja wanapata bidhaa yetu kwa wakati.
Space Engineering ina vipaumbele ambavyo inavizingatia kwa miaka mitatu kuanzia sasa, Kuongeza uzalishaji mara 3 ya sasa, Kutoka tani 4.5 hadi tani 13.5 Kuongeza majiko kutoka 450 hadi majiko 1500,Kuzalisha majiko madogo ya majumbani kutoka 0 hadi 1000 kwa mwezi Kuongeza majengo kwa ajili ya kuhidadhi bidhaa.